Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu ataka majibu yanayoeleweka kesi ya dawa za kulevya

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Mfaume Kiboko na mkewe, Pilly Mohamed Kiboko umedai jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).

Wakili wa Serikali, Daisy Makakala amedai leo Jumanne Machi 19, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba kuwa upelelezi bado haujakamilika na jalada lipo kwa DPP.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba amesema shauri hilo litakapokuja tena upande wa mashtaka waje na majibu yanayoeleweka ili wapate mwendelezo wa kesi hiyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 2, 2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Kiboko na mkewe wanakabiliwa na shtaka moja katika kesi ya uhujumu uchumi namba 29/2018, ambapo wanadaiwa kusafirisha dawa za ku?evya aina ya heroin zenye uzito wa gram 251.25.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Mei 23, 2018 eneo la Tegeta Nyuki, wilaya ya Kinondoni, walisafirisha dawa za ku?evya aina ya heroin gram 251.25.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz