Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu amnunulia nguo mtuhumiwa, aliwahi kuwanunulia unga wezi

Hakimu Adet Qd Hakimu amnunulia nguo mtuhumiwa wa kunajisi

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakimu mkuu wa Mombasa, Vincent Adet kwa mara nyingine tena ameonyesha mtu na ukarimu, licha ya kutwikwa jukumu la kutekeleza haki na sheria, ambapo wakati mwingine hutoa adhabu kali.

Hii ni baada ya kumnunulia nguo mapya mtuhumiwa aliyefika kortini akiwa amevali shati na suruali zilizoraruka.

Richard Christopher Odhiambo, ambaye anakabiliwa na shtaka la kunajisi, aliwasilishwa kizimbani huku sehemu ya mwili wake ukionekena kwa kuvalia nguo zilizoraruka.

Odhiambo alimuambia hakimu huyo kwamba maofisa wa gereza la Shimo La Tewa, walikataa kumpa nguo ndipo akavalia zilizoraruka na kuongeza kuwa maofisa hao wa gereza walisisitiza wanaweza kumpa mavazi ya wafungwa, baada ya kupewa hukumu rasmi, lakini kwa sasa bado.

Hakimu Adet aliwahi kuwachangia mke na mume waliofikishwa mahakamani kwa kosa la kuiba unga. Hakimu huyo alisema kwamba baada ya kuwasikiza wawili hao, aligundua kuwa walilazimika kuiba unga kwa sababu walikuwa na njaa.

Adet alipitisha harambee ya kuchangia ambapo shilingi 1,000 za Kenya (takribani Tsh 20,000) zilichangwa kortini na kukabidhiwa wawili hao, huku hakimu akiwataka wasirudie kitendo kama hicho tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live