Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu akwamisha kesi ya mawakala wa ATCL

61161 Pic+atcl

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi inayowakabili mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania  (ATCL) imeshindwa kuendelea baada ya hakimu anayeendesha shauri hilo kutokuwepo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa matatu likiwemo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh10,874,280.

Washtakiwa hao  ni Fabian Ishengoma, Adamu Kamara, Marlon Masubo, Alexander Malongo, Tunu Kiluvya, Jobu Mkumbwa, Mohamed Issa, Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega.

Wakili wa Serikali, Janeth Magoho amedai leo Jumatatu Juni 3, 2019 kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika hivyo ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameahirisha shauri hilo hadi Juni 16, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa matatu ambayo ya kuisababishia hasara shirika hilo, kutumia njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Pia Soma

Katika tarehe tofauti kati ya Machi10 na Oktoba 9 mwaka jana wakiwa maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Mwanza watuhumiwa hao waliisababishia shirika hilo hasara ya Sh10.87 milioni  huku wakijua kufanya hivyo ni kosa.

Shtaka la pili tarehe tofauti kati ya Machi10 na Oktoba 9 mwaka jana wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Mwanza watuhumiwa hao walitumia njia ya udanganyifu kujipatia kiasi cha Sh10.87 milioni kwa lengo la kuwakatia watu tiketi za ndege la shirika hilo .

Amedai katika shtaka la tatu la utakatishaji wa fedha katika tarehe tofauti kati ya Machi 10 na Oktoba 9 mwaka jana wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Mwanza watuhumiwa hao walijipatia Sh10.87 milioni ni mali ya shirika la ATCL huku wakijua ni kosa la kisheria

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz