Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima: Baada ya kujeruhi, Panya Road walichukuliwa na Noah nyeusi

Gwajima Panya Oad Gwajima baada ya kuwatembelea majeruhi wa Panya Road

Thu, 5 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima amesema katika mahojiano yake na majeruhi wa Panya Road amemueleza kuwa baada ya tukio vijana hao walichukuliwa na gari mbili nyeusi aina ya Toyota Noah.

Gwajima amehoji mmiliki wa magari hayo huku akitaka Jeshi la Polisi kufanyia kazi suala hili kwa kuwa inaonekana kuna mtu anawafadhili vijana hao

"Wakati nawahoji hawa waliojeruhiwa, nimezungumza na mmoja ambaye ni dereva maloro anasema baada ya tukio kufanyika hawa vijana walichukuliwa na Noah mbili nyeusi, sasa swali langu ni kwamba Noah ilikuwa ya nani?

"Kwa sababu baada ya tukio hilo likatokea lingine Mbweni, Polisi wafanye kazi inawezekana kuna mtu anawafadhili hawa vijana kwa lengo la kuharibu image ya serikali," Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live