Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita: Polisi wamkamata Imamu kwa uhalifu

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Geita, Safia Jongo.jpeg Geita: Polisi wamkamata Imamu kwa uhalifu

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Imam wa msikiti wa Nyankumbu mjini Geita, ambaye pia ni mwalimu wa madrassa, Abdulrahman Yassin akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari mjini Geita na kukanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Imam huyo ametekwa na watu wasiojulikana, bali yeye na wenzake walikamatwa na jeshi la polisi.

“Kutokana na aina ya tuhuma alizonazo, kulikuwa na watuhumiwa wengine ambao bado hawajakamatwa, hivyo suala la kukamatwa kwake ndio maana hatukuliweka wazi.

“Lakini baada ya kukamilisha ukamataji wa timu nzima ambayo ilikuwa inakabiliwa na tuhuma hizo, tumeamua tuliweke wazi kwamba Imam huyu anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

“Uchunguzi unaendelea, ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili hususani kujihusisha na matukio ya kihalifu,” amesema Kamanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live