Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gari la magereza lakwamisha kesi ya Seth na Rugemarila, Hakimu atoa maagizo

90655 Gari+pic Gari la magereza lakwamisha kesi ya Seth na Rugemarila, Hakimu atoa maagizo

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi inayowakabili Harbinder Seth, ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP na Mkurugenzi wa VIP Solution, James Rugemarila imeshindwa kuendelea baada ya usafiri wa kuwatoa gerezani kuwapeleka mahakamani kukosekana.

Mbali na  hao, mwingine kwenye kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni aliyekuwa mwanasheria wa kampuni ya  kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege ambaye yeye alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Desemba 20, 2019.

Rugemarila na Seth wao walifikishwa kwa mara ya kwanza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mwaka 2017.

Leo Alhamisi Januari 2, 2019, Wakili wa Serikali ya Tanzania, Gloria Mwenda wakati kesi hiyo ilipoitwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu amesema washtakiwa hao wameshindwa kufikishwa mahakamani kutokana na changamoto ya usafiri.

Hata hivyo, ameeleza kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kitajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Hakimu Chaungu ameiahirisha kesi hiyo mpaka Januari 16, 2020 na kuamuru siku hiyo washtakiwa hao wapelekwe mahakamani hapo.

">Makandege  katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2017  anakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuisababishia hasara Serikali ya dola za Marekani 980,000 na utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka hayo Desemba 20, 2019 baada ya kuunganishwa na washtakiwa Seth na Rugemarila katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Rugemarila na Sethi wanadaiwa kutenda makosa hayo katika jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao ni kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi.

Pia, wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha  na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh309 bilioni

Chanzo: mwananchi.co.tz