Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fundi umeme mbaroni kwa kumpiga shoti mwenzake

D0ZGC2YXQAE 9kO Fundi umeme mbaroni kwa kumpiga shoti mwenzake

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fundi umeme mkazi wa Dareda Mission Wilayani Babati Mkoani Manyara, anashikiliwa polisi kwa tuhuma za kumpiga shoti ya umeme fundi mwenzake baada ya kumuibia.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Benjamin Kuzaga akizungumza na Mwananchi Digital Disemba 14 amesema tukio hilo limetokea Disemba 11 eneo la Dareda.

Kamanda Kuzaga amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Baraka Finda (30) mkazi wa Dareda Mission Wilayani Babati.

Amesema mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kwa kosa la kumjeruhi kwa kumpiga shoti ya umeme fundi mwenzake aitwaye Baraka John (23).

"Mtuhumiwa huyo alimfunga mwenzake mikono na miguu na kumziba mdomo kisha kumpeleka nyumbani kwake na kuchomeka waya wa umeme na kuanza kumpiga shoti mwili mzima," amesema.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa huyo kudai kuwa fundi mwenzake ameiba baadhi ya vifaa vyake vya kazini.

Amedai kuwa majeruhi huyo alikimbizwa hospitali ya misheni ya Dareda kwa matibabu na baadaye aliruhusiwa kupumzika nyumbani.

"Polisi tunaendelea na upelelezi wa tukio hilo na pindi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili akajibu shtaka," amesema kamanda Kuzaga.

Mmoja kati ya shuhuda wa tukio Dismas Peter amesema tukio hilo limewasikitisha mno kwani John hakupaswa kufanya hivyo hata kama amekosewa na fundi mwenzake.

"Hivi sasa tupo kwenye mgao wa umeme wakati huyu fundi anauchezea kwa kumsababishia matatizo kwa kutaka kumuua mwenzake na umeme," amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live