Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fundi nguo asimulia alivyotekwa, adai kuibiwa Sh5milioni

60378 Pic+fundi

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Fundi nguo na muuza vitambaa vya suti katika soko la Mugumu wilayani Serengeti, Juma Siki (34) aliyetekwa Jumamosi iliyopita na kupatikana Jumatatu Mei 27, 2019 amesema waliomfanyia kitendo hicho walimpora Sh4.9milioni , kadi za benki na simu ya mkononi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Mei 29, 2019 Siki aliyepatikana wilayani Bunda amesema waliomteka walimvamia wakiwa na bastola na mapanga.

"Cha kwanza walitaka fedha, simu na kadi mbili za benki na kuniomba namba za siri. Katika akaunti yangu kulikuwa na Sh4.9milioni nilizokuwa nataka kuchukua mzigo,” amesema.

Amesema  alivyoingizwa katika gari jeusi alilodai kuliona kabla ya kutekwa, alifungwa kitambaa usoni na hakujua alikokuwa akipelekwa, “Hadi siku nimetupwa eneo la machinjio ya Bunda na kujisalimisha polisi.”

Amebainisha kuwa alipigwa kichwani na panga na kufungiwa ndani ya chumba kidogo akiwa chini ya ulinzi akisubiri watekaji hao kutumiwa fedha walizohitaji.

Jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alilieleza Mwananchi kuwa Ndaki alipatikana Jumatatu, “Amepatikana jana (juzi) usiku alifika polisi Bunda kwa Bodaboda akapelekwa hospitali kwa matibabu, sasa hivi tunaendelea na mahojiano atueleze mkasa mzima."

Habari zinazohusiana na hii

Taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu wa Siki zinaeleza kuwa hakuwa katika hali mbaya ya kiafya siku aliyopatikana.

“Alitueleza kuwa alipigwa na ubapa wa panga kisha akafungwa kitambaa usoni. Amesema alijikuta sehemu ambayo haitambui na aliomba msaada wa Bodaboda hadi polisi," amesema mmoja wa ndugu zake.

Baada ya kutekwa kwa Saki, Kamanda Ndaki alisema wanafuatilia kubaini wahusika kupitia simu yake ambayo imetumika kutuma ujumbe kwa rafiki yake ukimtaka atumiwe Sh15 milioni ndipo wamuachie huku ukieleza kuwa bado yupo hai.

Alieleza kuwa  ndani ya gari ya Saki aina ya Toyota Noah lililokutwa karibu na nyumba yake walikuta damu, kisu, mawe na vitu vingine ambavyo inadaiwa vilitumiwa na watuhumiwa wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu alilieleza tukio hilo akidai limewastua na askari wanaendelea na ufuatiliaji na ameomba watu wenye taarifa sahihi wasaidie ili watuhumiwa waweze kukamatwa.

Sirikwa Marwa aliyedai ni rafiki mkubwa wa  Juma alikiri kupokea ujumbe wa simu kupitia namba ya rafiki yake ukimtaka ajitahidi kutuma kiasi hicho cha fedh

Chanzo: mwananchi.co.tz