Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Festo akamatwa akidaiwa kumuua mchepuko wake na mtoto

Maxresdefault 1 950x534 1 660x400 Festo akamatwa akidaiwa kumuua mchepuko wake na mtoto

Tue, 15 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja Festo Venance mwenye umri wa miaka 38 kwa tuhuma za kuwaua watu wawili na kumjeruhi mwingine mmoja, katika kijiji cha Kumzuza wilayani Ngara.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amewataja waliouawa kuwa ni Magreth Jacob mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa hawara wa mtuhumiwa na mtoto mdogo Jonam Niyonzima mwenye umri wa miaka mitatu, huku aliyejeruhiwa akitajwa kuwa ni Penina Joseph Mwenye umri wa miaka 40, ambaye amelazwa katika hospitali ya Murgwanza wilayani humo.

Kamanda huyo amesema kuwa sababu ya mauaji hayo bado haijafahamika na mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa lakini bado hajakiri kuhusika na mauaji hayo, ingawa kuna baadhi ya mazingira yanaonyesha kuhusika kwake, ikiwamo nguo alizokuwa amevaa kukutwa na damu.

MUWASA YAPEWA WIKI MOJA KWA KUSAFISHA MABWAWA YA MAJI TAKA

Chanzo: millardayo.com