Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fedha miradi ya maji zawasweka ndani watatu

Cruiser Polisi.jpeg Fedha miradi ya maji zawasweka ndani watatu

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia viongozi watatu wa kamati ya jumuiya ya maji inayosimamia mradi wa maji wa Mharamba uliopo wilayani Geita, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha wanazokusanya kwa wananchi kwa kuwauzia maji kwa kipindi cha miaka sita.

Viongozi hao walikamatwa mara baada ya kushindwa kujitetea juu ya matumizi ya fedha mbele ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipowauliza kuhusu kiasi kilichopo kwenye akiba ambacho kilitakiwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 20 ndipo akaamua kuvunja kamati hiyo.

Baada ya waziri kuvuja jumuiya hiyo Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Joseph Musukuma ameomba viongozi hao wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengine  huku mkuu wa wilaya hiyo  akiagiza kamati ya ulinzi kuwakamata kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

"Yaani watu unapiga hesabu milioni 20 halafu wana laki tano halafu wanachekacheka namna hii, mimi ni mbunge na tunamuheshimiwa DC hawa watu lazima watoe hesabu kama hawana kamata hatuwezi kuwa wapole hivyo, lazima washughulikiwe hawa wezi kama wezi wengine," amesema Mhe. Msukuma.

Mradi wa maji wa Mharamba umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na ulikabidhiwa kwa kamati hiyo mwaka 2015 na unakadiriwa kuhudumia wananchi zaidi ya 4,000 wa kata ya Nkome.

Chanzo: eatv.tv