Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya kijana aliyejinyonga Moshi yaandamana

16001 Mwanafunzi+pic TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi.Familia ya mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Rau, Emmanuel Tarimo (18) aliyejinyonga baada ya kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake a kidato cha kwanza, wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa shule hiyo kutaka kujua sababu za mwanafunzi huyo kuhojiwa hadi kupelekea kujiua.

Dada wa mwanafunzi huyo, Tedy Maro amesema anataka uongozi wa shule hiyo uwaeleze kinagaubaga kwanini walimu wa shule hiyo wamtuhumu mwanafunzi huyo wakati wao familia hawakupewa taarifa zozote kuhusu mwenendo wa tabia za mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo alijinyonga hadi kufa Septemba 4, mwaka huu nyumbani kwao Kijiji Cha Rau, mtaa wa Saba Saba baada ya kutuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi mwenzake wa kidato cha kwanza.

Mazishi ya kijana huyo yanatarajia kufanyika kesho Moshi.

Soma Zaidi:

VIDEO: Mwanafunzi ajinyonga baada kutuhumiwa kumpa mimba mwenzake

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz