Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FCC kufanya utafiti namna bora kudhibiti wizi wa mtandaoni

Dreamstime M 138605425 Matukio ya uhalifu mtandaoni yamekua yakiongezeka kila kukicha duniani kote

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeiagiza Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) kufanya utafiti ili kupata mifumo bora ya kuzuia wizi wa fedha kwa njia ya mtandao hapa nchini.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji aliyekuwa akizungumza katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Kumlinda Mtumiaji Duniani jijini Mwanza amesema bado jamii inasumbuliwa na ulaghai na wizi wa kimtandao na kwamba FCC kwa kushirikiana na vyombo vingine wafanye utafiti wa kina ili kukabiliana na janga hilo la kitaifa na kidunia.

Amesema ili watu wawe salama katika utumiaji wa huduma za mtandaoni hasa za kifedha wainapaswa kufuata mifumo imara iliyowekwa na Serikali.

Aidha, Waziri huyo amewataka watoa huduma za fedha wote kuweka mifumo itakayolinda watumiaji ambao ni wateja wao.

Kuhusu masuala ya ukatatishaji fedha pamoja na ugaidi duniani yanayofanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vyombo vilivyopewa dhamana kusimamia sheria vinatakiwa kuliona hilo na kuliwekea misingi imara ya kupambana nalo.

"Utakatishaji wa fedha unaharibu kabisa uchumi wa nchi na suala hili ni lazima kama nchi tupambane nalo ili kulimaliza katika jamii yetu,'' amesema Dk Kijaji.

Amepongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuendelea kuwa na mifumo imara ya kulinda watoa huduma za fedha wa ndani na nje nchi.

Ifikapo mwaka 2024 inakadiriwa kuwa watu bilioni 3.6 duniani kati ya bilioni 7 watakuwa wanatumia huduma za fedha kwa njia ya kidigitali, hivyo ulinzi wao ni muhimu ili kuendelea kufaidika na fursa za kidijitali.

Mwenyekiti wa bodi ya FCC, Dk Agrey Mlimuka amesema, wataendelea kusimamia haki katika ushindani ya kibiasahara nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live