Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Erick Kabendera alivyopokea taarifa kifo cha mama yake, kuzikwa Kagera

90457 Kabendera+pic.png Erick Kabendera alivyopokea taarifa kifo cha mama yake, kuzikwa Kagera

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Almachus Kabendera amesema mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mama yake mzazi, Verdiana Mujwahunzi.

Verdiana (80) amefikwa na mauti leo Jumanne Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Amana, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa siku mbili kwa ajili ya matibabu.

Almachus ambaye ni baba mdogo wa Erick akizungumzia alivyompelekea taarifa mwandishi huyo aliyeko rumande katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam amesema ulikuwa ni wakati mgumu kumfikishia taarifa hizo na alipopewa alijawa na huzini na kutokwa machozi.

“Wengi tunajua msiba wa mama unavyoshtua na yeye alipokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa lakini tukajaribu tukaongea naye na kumweka sawa na sisi tulijitahidi kumuweka sawa kwa kuzungumza naye na sisi tunaendelea na taratibu za mazishi,” amesema Almachus

Kuhusu ratiba ya msiba, Almachus amesema wanatarajia kuaga mwili wa Verdiana Ijumaa ya Januari 3, 2020 Dar es Salaam na baadhi ya ndugu wataanza safari kwenda Kagera huku mwili ukisafirishwa Jumamosi ya Januari 4, 2020 kwa ndege.

Amesema mazishi ya Verdiana yatafanyika Januari 6, 2020 katika kijiji cha Katoma, wilaya ya Bukoba mkoni Kagera

Erick yuko rumande tangu alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 ambapo alisomewa mashtaka matatu ambayo ni kupanga na kushiriki mtandao wa uhalifu, kukwepa kodi zaidi ya Sh173 milioni na utakatishaji fedha zaidi ya Sh173 milioni.

Mashtaka hayo hayana dhamana na amekuwa gerezani kwa kipindi chote wakati kesi yake ikiendelea.

Chanzo: mwananchi.co.tz