Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Duuuh! Jamaa adakwa na bangi tani moja, polisi waeleza

Bangii Kigomaaa Duuuh! Jamaa adakwa na bangi tani moja, polisi waeleza

Fri, 15 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani humo imemtia mbaroni mtu mmoja mkulima na mkazi wa kijiji cha Kabulanzwili wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma akituhumiwa kupatikana na madawa ya kulevya aina ya bangi yanayokadiriwa kuwa na uzito wa tani moja.

Kamanda mkoa Kigoma Ramadhani Kingai akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma alimtaja mtu aliyekamatwa kuwa ni Lije Nicholous maarufu kama Madeberi (48) mkulima na mkazi wa kijiji cha Kabulanzwili wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Kamanda kingai alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa na polisi waliokuwa doria akiwa kwenye harakati za kusafirisha madawa hayo ya kulevya kwenda kuuza ambapo haijalezwa mara moja yalikuwa yakipelekwa wapi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live