Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dunia imekwisha! Daktari wa zahanati adaiwa kubaka mtoto

Rape ED Daktari wa zahanati adaiwa kubaka mtoto

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wakati mwarobaini wa matukio ya ukatili dhidi ya watoto ukiendelea kuwa kitendawili kisichoteguka, mtoto wa miaka minane anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Golani mkoani hapa (jina limehifadhiwa), anadaiwa kubakwa na anayedaiwa kuwa daktari wa Zahanati ya Kimara Wilaya ya Ubungo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, akifafanua kuwa bado uchunguzi unaendelea kufanyika.

“Taarifa za kubakwa tunazo lakini wapi, amefanya nani, bado tunafanya uchunguzi, hadi sasa mtuhumiwa ameshakamatwa na uchunguzi unaendelea,” alisema Kamanda Muliro.

Kwa mujibu wa baba wa mtoto huyo, Yohana Hema, mwanawe alikumbwa na tukio hilo alipokuwa anacheza kwenye nyumba ya daktari huyo iliyo karibu na nyumbani kwao.

“Hatukugundua haraka, wiki mbili baada ya tukio hilo, mtoto alimhadithia rafiki yake kilichomtokea na yule mtoto akaenda kumhadithia mama yake,” alisema.

Yohana alilieleza Mwananchi kuwa baada ya mzazi huyo kupata taarifa alimtaarifu mama mzazi wa mtoto huyo (mkewe), hivyo waliwaita watoto wote kwa mahojiano.

Baada ya mahojiano na mtoto, alithibitisha kufanyiwa kitendo hicho, ambacho pia kilithibitishwa na mtoto wa mtuhumiwa, kwani aliona wakati tukio linafanyika.

“Maelezo yao wanasema alimtupa kitandani akawa anamfanyia kitendo hicho na alikuwa analia,” alisema.

Taarifa za kubakwa kwa mwanawe alipewa Julai 18, mwaka huu na ndipo alipokwenda Kituo cha Polisi Gogoni kwa ajili ya kupata Fomu namba 3 kisha kwenda hospitali kupima ili kuthibitisha.

Baada ya kupata fomu hiyo, alifafanua kuwa walikwenda hospitali na vipimo vimeonyesha kwamba mtoto alikuwa na michubuko. “Lakini nilipata changamoto katika ujazaji wa PF3 maana daktari alikuwa ananizungusha, akadai inatakiwa ijazwe baada ya wiki tatu, tulisumbuana na baadaye aliijaza.’’

Alisema tayari mtuhumiwa ameshakamatwa na amefikishwa katika Kituo cha Polisi Gogoni kwa hatua zaidi.

“Hapa nipo Gogoni na mashahidi tumeitwa hapa Polisi baada ya kusikiliza, ndiyo tutajua kama lini tunakwenda mahakamani,” alisema mzai huyo.

Alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mtafilo Kipingu alisema kwa taarifa zaidi atafutwe Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

“Mpigie Kamanda wa Kanda Maalumu ndiye atakayezungumzia tukio hili,” alisema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz