Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dudu Baya anashikiliwa Oysterbay

44172 Dudupic Dudu Baya anashikiliwa Oysterbay

Thu, 28 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanamuziki Godfrey Tumaini maarufu  ‘Dudu Baya' anashikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema Msanii huyo anashikiliwa kwa mahojiano.

Dudu Baya aliyewahi kutamba na wimbo Mwanangu Huna Nidhamu, alijisalimisha leo Februari 28, 2019 baada ya kuamriwa na Baraza la Sanaa la Taifa kufanya hivyo.

Jana, Waziri wa Habari na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliagiza Jeshi la Polisi na Basata wamchukulia hatua mwanamuziki huyo kwa makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba.

Baada ya amri hiyo, Basata ilimtaka mwanamuziki huyo kujisalimisha katika kituo cha polisi Oysterbay asubuhi ya leo.

Mwanamuziki huyo ameshtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao.

MWAKYEMBE AAGIZA DUDU BAYA AKAMATWE, MWENYEWE ASEMA HAJALI



Chanzo: mwananchi.co.tz