Mahakama moja nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha miezi 18 mama mmoja kwa kosa la kumtesa mtoto wake wa miaka miwili kwa ukatili, unyama na kumdhuru mwili.
Mahakama moja nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha miezi 18 mama mmoja kwa kosa la kumtesa mtoto wake wa miaka miwili kwa ukatili, unyama na kumdhuru mwili. Mama huyo mwenye umri wa miaka 28 Dorothy Nabulime atatumikia kifungo cha miezi 18 jela kwa kosa la ukatili na unyama kwa mtoto wake na kifungo cha miezi sita kwa kosa la kumdhuru mtoto wa miaka miwili lakini adhabu hizo mbili zitatolewa kwa wakati mmoja. Hakimu Mkuu aliiambia Mahakama siku ya Jumanne.