Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Donge nono kutolewa watakaofichua walioua simba sita

3da7be06c19322b403763c2e0c0a122a Donge nono kutolewa watakaofichua walioua simba sita

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Usimamizi Wanyamapori Uganda (UWA) imetangaza zawadi ya Sh milioni 10 kwa mtu atakayewezesha kupatikana taarifa ya watu waliohusika kuua simba sita katika mbuga ya taifa ya Qeen Elizabeth.

Taarifa ya UWA iliyotolewa hivi karibuni inaeleza kuwa, kuhifadhi rasilimali za wanyamapori ni wajibu wa wananchi wote ambao wanapaswa kufanya kazi pamoja kupambana na aina zote za uhalifu kwa wanyamapori.

“Kwa hivyotunawasihi umma kuungana nasi katika vita hii kwa kutupa habari za uhakika ili wauaji wa simba wetu wapatikane,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

"Tunaomba yeyote aliye na habari muhimu awasiliane nasi ,na tunawahakikishia kuwa tutafanya siri kwa mtu yeyote ambaye atatupa habari."

Alisema tangu walipogundua kuuawa kwa simba hao Machi 18, mwaka huu, wamekusanya sampuli kutoka mizoga ya wanyama hao na kuzichukua kwa uchunguzi wa maabara ili kujua sababu ya vifo hivyo na matokeo yatakapotoka yatatolewa kwa umma.

Siku moja baada ya tangazo hilo, timu ya ulinzi na usalama ilikamata watu wanne wanaodhaniwa kuwapa sumu simba hao na kisha kuondoka na viungo ikiwamo vichwa, miguu na moyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kanungu, Hajji Shafque Sengooba alithibitisha kukamatwa kwa watu hao wanne wakiwa na vichwa vya simba katika makazi yao.

Chanzo: www.habarileo.co.tz