Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Dogo’ atupwa jela miaka 60 kumbaka mama miaka 56

7f479f7b50bcd3d8e7f21775d56acad3 ‘Dogo’ atupwa jela miaka 60 kumbaka mama miaka 56

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma imemhukumu kifungo cha miaka 60 jela, Daudi Samson (22) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanamke mwenye umri wa miaka 56 (majina yanahifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali ikiwamo kumvunja mgongo.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Stanley Mwakihaba alisema upande wa mashtaka ambao jana uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Tawabu Issa, ulipeleka mashahidi watano ambao walisikilizwa na mahakama hiyo.

Alisema miongoni mwa mashahidi hao ni daktari aliyemhudumia mlalamikaji katika kesi hiyo ya Jinai Namba 16 ya Mwaka 2021.

"Ushahidi wa daktari na PF 3 ulithibitisha alibakwa, alilawitiwa na kuvunjwa mgongo na mahakama ilielezwa kuwa hali ya mgongo ililazimu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kumpa rufaa akatibiwe Hospitali ya Bugando," alisema Hakimu.

Alisema hayo yalitokea usiku wa Desemba 25 mwaka jana, baada ya Daudi kumvizia mwanamke huyo vichakani wakati akienda msibani.

Alisema mlalamikaji aliieleza mahakama kuwa alimtambua aliyemtendea ukatili huo na kumtaja kwa majina na kwamba wakati akimbaka na kumlawiti alikuwa akitishia kumuua kwa kumchinja kwa kutumia kisu alichokuwa amekishikilia.

"Nililia sana nikamwambia Daudi kwa nini unanifanyia haya katika utu uzima huu nilionao, wewe si ni sawa na wanangu? Lakini hakunihurumia, aliendelea tu huku akinitaka ninyamaze la sivyo angeniua," alisema mama huyo wakati alipotoa ushahidi wake.

Mshitakiwa wakati akijitetea alikana kutenda makosa hayo na kwamba hata mashahidi waliomtaja walitumia maneno ya kusikia kwa mlalamikaji. Kwa upande wake hakupeleka shahidi hata mmoja.

Hakimu Mwakihaba alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili, mahakama ilijiridhisha pasi na shaka kwamba mlalamikaji alibakwa, alilawitiwa na kuvunjwa mgongo.

Wakati huohuo, Mahakama hiyo imemhukumu Mtao Mgori kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa sekondari (majina yanahifadhiwa) huku yeye akiwa hayupo mahakamani.

Licha ya hukumu hiyo, Hakimu Mwakihaba aliieleza mahakama jana kwamba mshtakiwa aliruka dhamana na hivyo wadhamini wake, Nyanjala Mlungu na Julius Mtao wote wakazi wa Kigera Etuma, Wilaya ya Musoma, wanatafutwa.

Hukumu hiyo ya Kesi ya Jinai Namba 100 ya Mwaka 2020, ilielezwa na Hakimu Mwakihaba kuwa utekelezaji wake utaanza baada ya mhukumiwa kupatikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live