Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dodoma: Mtoto wa Miaka 11 Ajinyonga

Nyuki Pic Data Dodoma: Mtoto wa Miaka 11 Ajinyonga

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

NI SIMANZI na huzuni kubwa baada ya mtoto Leila Selemani Kitenge mwenye umri wa miaka 11, ambaye jana November 4, 2021 amekutwa amefariki kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni kujinyonga.

Mtoto Leila ambaye alikuwa akisoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Chang’ombe B, alikuwa akiishi na babu na bibi yake katika Mtaa wa Usomalini, Chang’ombe jijini Dodoma.

Imeelezwa kuwa, mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umening’inia huku shingo yake ikiwa imefungwa na kitambaa cha nguo kwenye nguzo ya kuanikia nguo ndani ya uzio wa nyumba alipokua akiishi na wazee wake hao.

Akizungumzia tukio hilo, babu wa marehemu amesema kwamba bado wanaendelea kufuatilia kujua kama mjukuu wao alikusudia kujiua kwani kwa mujibu wa mashuhuda wa kwanza kufika eneo la tukio wanadai walimkuta tayari ananing’inia na chini kuna ndoo huku mazingira ya kamba yakiwa ya kitanzi.

Mwili wa Marehemu Leila umesafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.

(Picha si ya tukio husika)

Chanzo: globalpublishers.co.tz