Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Pima na wenzake waachiwa huru baada ya kushinda rufaa

Dk Pima Na Wenzake Waachiwa Huru Baada Ya Kushinda Rufaa Dk Pima na wenzake waachiwa huru baada ya kushinda rufaa

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili wameshinda rufaa waliyokata kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imesomwa leo Ijumaa, Februari 16, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna.

Mbali na Dk Pima, wengine walioachiwa huru ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Chanzo: Mwananchi