Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Pima na wenzake kukata rufaa

Dk Pima Na Wenzake Kukata Rufaa Dk Pima na wenzake kukata rufaa

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili, wanatarajia kukata rufaa baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5/2022, mbali na Dk Pima watuhumiwa wengine ni aliyekuwa Mwekahazina wa Jiji hilo, Mariam Mshana na aliyekuwa mkuu wa idara ya mipango, takwimu na ufuatiiaji, Innocent Maduhu.

Agosti 31, 2023 Dk Pima na wenzake walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa makosa tisa yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo utakatishaji fedha Sh103 milioni.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumatatu Septemba 4, 2023 kwa simu, mmoja wa mawakili waliokuwa wanawatetea watuhumiwa hao, Sabato Ngogo amesema watakata rufaa na wanatarajia kuwa na sababu zaidi ya 15.

"Tutakata rufaa kwa kishindo kikubwa sana, tuliambiwa tunapewa nakala ya hukumu leo hii Jumatatu, tutaisoma na kesho au kesho kutwa tutakuwa tumewasilisha notisi ya nia ya kukata rufaa,"amesema wakili huyo na kuongeza;

"Tutahakikisha tunapata mwenendo wa kesi mapema na haraka iwezekanavyo. Sababu za rufaa tunazo tayari na tunazo zaidi ya sababu 15.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live