Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mabula aahidi kuboresha Elimu

C2847d94c42e8d21032e818dabe3489b Dk Mabula aahidi kuboresha Elimu

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk Angelina Mabula amewahidi wakazi wa kata ya Ibungilo kuwa ataboresha sekta ya Elimu katika kata yao.

Dk Mabula alitoa ahadi hiyo wakati alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya tenki la maji. Alisema Serikali ya CCM imetenga shilingi milioni 75 kwajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Kiloleli na Kilimahewa. Dk Mabula alisema pia watajenga matundu ya vyoo katika shule ya msingi Nyamanoro na bajeti ya ujenzi huo ni milioni 11/-.

Alisema wametenga milioni 30 kwajili ya ujenzi wa chumba cha mahabara katika shule ya sekondari Ibungilo. Aliwapongeza wakazi wa Elimu kwa msaada wao wa hali na mali katika kusaidia wilaya yao ambapo imekuwa ikifanya vyema katika mitihani ya kitaifa.

Dk Mabula alisema wamefanikiwa kutatua migogoro ya Ardhi katika maeneo ya Mhonze na Jiwe kuu ambapo watu wote wamelipwa fidia.

Alisema katika sekta ya Ardhi jumla ya wakazi 930 wamechukua hati na kurasimishiwa maeneo yao. Alisema katika kero ya maji,Serikali imetenga bilioni 77 kwajili ya ujenzi wa miradi ya maji wilayani Ilemela.

Mgombea udiwani kupitia CCM katika kata ya Ibungiro,Magera Hussein aliahidi endapo akishinda atashirikiana na Dk Mabula katika kusaidia ujenzi wa Zahanati katika eneo lao

Chanzo: habarileo.co.tz