Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Kitenge kortini akituhumiwa kumpapasa matiti mgonjwa

10653 Matiti+pic TanzaniaWeb

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Daktari wa Hospitali ya Tumaini ya jijini hapa August Freeman (51) maarufu Kitenge amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu shtaka la kumshika matiti mgonjwa.

Dk Freeman alipandishwa mahakamani hapo leo Julai 3 na kusomewa shtaka moja la kumdhalilisha mwanamke kingono.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto amedai mbele ya hakimu mkazi, Flora Mjaya, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria.

Slyvia amedai kuwa Julai 18, 2017 katika Hospitali ya Tumaini, Dk Freeman alimdhalilisha mwanamke mwenye miaka 31 ambaye alifika  hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Amedai kuwa siku ya tukio, mshtakiwa alimshikashika matiti mwanamke huyo ambaye alikwenda katika hospitali hiyo kupata matibabu, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mshtakiwa amekana kuhusika na shtaka hilo na hakimu Mjaya alitoa masharti ya dhamana yakiwa ni kuwa wadhamini wawali kutoka sekta inayotambulika kisheria watakaosaini hati yenye thamani ya Sh2 milioni kila mmoja.

Mshtakiwa alitimiza masharti yupo nje kwa dhamana, hakimu Mjaya aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 24 mshtakiwa atakaposomewa maelezo ya awali (PH).

 

Chanzo: mwananchi.co.tz