Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Chegeni, Polisi wavutana

24606 Pic+chegeni TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Busega (CCM) Dk Rafael Chegeni amesema hajawahi kukamatwa polisi na wanaoeneza uzushi huo wana lengo la kumchafua.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema jeshi hilo halina sababu ya kusema mtu kwa ubaya lakini ukweli ni Dk Chegeni alikuwapo eneo la tukio.

Jana, taarifa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimtaja Chegeni na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kwamba walikamatwa mkoani Mbeya kwa kosa la kuharibu mali za mwekezaji.

"Hapa nimepigiwa simu hadi nimechoka, niko Mwanza ninafanya shughuli zangu na za jimbo langu, imeniuma sana na kunipa shida kubwa," amesema Dk Chegeni.

Mbunge huyo amesema taarifa hizo hazihusiani na yeye  kwani yeye si mwanasheria hivyo kuhusishwa katika jambo ambalo liliwahusu watu wa sheria ni kumdhalilisha.

"Mfano Masha ni mwanasheria, huenda alikuwa akitimiza wajibu wake kisheria, mimi naingiaje hapo,” amesema Dk Chegeni.

Kamanda Matei akizungumza leo Jumatatu na Mwananchi amesema: “Umeniambia amekupigia simu kukanusha au?”

Alipoelezwa kwamba Dk Chegeni amekanusha baada ya kuzungumza na Mwananchi, Kamanda Matei amesema: “Sasa mzee fuata kile polisi walichokisema na si yeye. Huyu anaitwa Dk Raphael Chegeni ni mbunge wa Busega alikuwapo eneo la tukio na maelezo ameandika, ningekusomea lakini maadili hayaruhusu.

“Kwa nini tusimtaje mtu mwingine, tukamtaje yeye,” amehoji Kamanda Matei.

Chanzo: mwananchi.co.tz