Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani ajinyonga kwa kutumia mtandio

33576 Pic+ajinyonga Tanzania Web Photo

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

                          

Unguja. Asha Ali Abei (55), diwani wa zamani wa kata ya Nyerere amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 26, 2018.

Akizungumza leo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Kheri Musa amesema marehemu ambaye kwa miaka ya nyuma alikuwa diwani, alikutwa amekufa kwa kujinyonga akitumia mtandio alioufunga katika dirisha, tukio lililotokea katika shehia ya Magomeni.

Baadhi ya majirani wa marehemu walisema kwamba walipata taarifa za kifo hicho asubuhi baada ya mtoto wa marehemu kupiga kelele.

Tatu Amme, amesema huenda jirani yake alijinyonga kutokana na msongo wa mawazo kwa madai kuwa wiki iliyopita alionekana kutokuwa na raha akidai huenda alikuwa akikabiliwa na madeni mengi.

Sheha wa shehia ya Magomeni, Rajab Ali Ngauchwa amesema si vyema wananchi kuchukua hatua za haraka katika mambo yanayowachanganya

Amesena ni vyema  familia kukutana na kujadili na kupata ili ufumbuzi wa tatizo kuliko watu kuchukua uamuzi kama huo wa kujitoa uhai.



Chanzo: mwananchi.co.tz