Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diwani ahukumiwa miezi sita jela

Law 1063249 1920 A35e082d75c748e18bf8108733914dc1 660x400 Diwani ahukumiwa miezi sita jela

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: mwananchi

Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Morogoro, Lucas Lemomo, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingiza mifugo kwenye mashamba na kuharibu mazao ya wakulima.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Tarafa ya Ngerengere, Godfrey Ng'itu, ameridhika kuwa mwezi Agosti mwaka huu mshtakiwa aliingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima watatu kwa makusudi na kuharibu mazao yao.

Ushahidi unaonesha kuwa moja ya shamba aliloharibu mshitakiwa huyo ambaye ni mfugaji wa jamii ya kimasai ni lenye mboga aina ya matembele na mahindi, vyote vikiwa na thamani ya Sh79,000.

Mfugaji huyo alidaiwa pia kuharibu shamba la mkulima mwingine lilikuwa na mahindi, kunde na mbaazi vyenye thamani ya Sh240,000.

Chanzo: mwananchi