Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva wa daladala mbaroni kwa tuhuma za kumuua kondakta

Majambazi Muliro Dereva wa daladala mbaroni kwa tuhuma za kumuua kondakta

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata, Maarifa Matala (45), dereva wa daladala kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake, Sharifa Nyamaishwa (31), ambaye ni kondakta wa daladala.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum, ACP Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa alimshambulia sehemu mbalimbali za mwili na kumuua.

"Tukio hilo limetokea tarehe 16 Agosti 2022, huko maeneo ya Kimara Suka, na mara baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoweka.

"Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hiyo lilianza upelelezi na ufuatiliaji wa haraka na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mkoani Lindi alipokuwa amejificha,"ameeleza.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa wapenzi hao walikuwa na migogoro inayosababishwa na wivu wa kimapenzi na kusababisha kugombana mara kwa mara, na mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha.

Ameeleza kuwa uchunguzi wa shauri hilo unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live