Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva wa basi la Sauli afungiwa leseni kwa miezi sita

Sauli Ed Dereva wa Basi la kampuni ya Sauli

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

KAMANDA wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini SACP Wilbroad Mutafungwa, amemfungia leseni Dereva wa Basi la kampuni ya Sauli kwa muda wa miezi sita kutokana na kitendo chake cha kuyapita (Overtake) magari mengine bila kuchukua tahadhari leo Agosti 23, wakati akitoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma na kusababisha ajali iliyojeruhi watu wanne.

KAMANDA wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini SACP Wilbroad Mutafungwa, amemfungia leseni Dereva wa Basi la kampuni ya Sauli kwa muda wa miezi sita kutokana na kitendo chake cha kuyapita (Overtake) magari mengine bila kuchukua tahadhari leo Agosti 23, wakati akitoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma na kusababisha ajali iliyojeruhi watu wanne. Mutafungwa amesema kitendo hicho kilichofanywa na Dereva huyo ni ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na ameeleza kuwa Dereva huyo atatakiwa kukaa bila leseni kwa muda wa miezi sita na kurudi tena darasani.

Chanzo: ippmedia.com