Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva teksi kortini akidaiwa kuhusika kutekwa kwa Mo Dewji

60102 Moopic

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Dereva teksi, Mousa Twaleb (46) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Mei 28, 2019 akikabiliwa  na mashtaka matatu likiwemo la  kumteka mfanyabiashara, Mohamed Dewji ‘Mo’.

Twaleb wamefikishwa mahakama hapo na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Mo alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11, 2018 wakati akifanya mazoezi katika Hoteli ya Colosseum iliyopo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, alipatikana Oktoba 20 katika eneo la Gymkhana baada ya kudaiwa kutelekezwa na watekaji hao.

Watu 12 walikamatwa na polisi katika tukio hilo wakihusishwa na watekaji.

Familia ya Dewji iliahidi kutoa Sh1 bilioni kwa mtu yeyote ambaye angetoa taarifa ambazo zingesaidia kupatikana kwa kijana wao. Hata hivyo hakuna aliyepata fedha hizo baada ya kupatikana kwake.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi kutoka mahakamani

Habari zinazohusiana na hii

 

Chanzo: mwananchi.co.tz