Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva bodaboda auawa na kuporwa pikipiki usiku

PANGA Dereva bodaboda auawa na kuporwa pikipiki usiku

Sat, 23 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwendesha pikipiki aliyetambuliwa kwa jina la Titus Pelamiho (38) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika mji wa Makambako mkoani hapa.

Hayo yamesenmwa jana Machi 22, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga wakati akizungumza nasi kuhusu tukio hilo, akisema marehemu alikuwa dereva wa pikipiki aina ya Kinglion ambayo pia imechukuliwa na watu wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo.

Amesema tukio hilo limetokea Machi 20, 2024 majira ya saa 2 usiku, ambapo bodaboda huyo alikutwa akiwa na majeraha ya kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na kwenye sikio la upande wa kulia.

Amesenma katika tukio hilo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili, huku likiendelea na uchunguzi na kuwahoji kuhusiana watu hao na tukio hilo la kinyama.

"Yeye alikuwa dereva wa pikipiki aina ya Kinglion ikiwa imechukuliwa na thamani yake ni Sh2.7 milioni. Tunaendelea na uchunguzi watu wawili tumewakamata," amesema Banga.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Matema uliopo Kata ya Maguvani, Thomson Mathai Nziku amesema alipigiwa simu na mjumbe wa nyumba 10 na ndipo alikwenda kushuhudia mwili wa marehemu.

"Ninatoa angalizo kwamba bodaboda wawe makini wanapoondoka kuelekea mahali hasa wakati wa usiku, wahakikishe wanakuwa na mtu anafuatana naye maana hatujui mtu anayemchukua ni mwema au siyo mwema," amesema Nziku.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Bodaboda Mji wa Makambako, Yusuph Mtelesi amesema marehemu alikuwa mwanachama wao na alikuwa anafanya kazi kituo cha soko jipya Maguvani.

"Tunachotambua sisi mwenzetu ameuawa ila ameuawa na nani hatufahamu, lakini ni kweli dereva bodaboda mwanachama wetu na alijiunga Januari mwaka 2023," amesema Mtelesi.

Amewataka madereva wa boda boda Halmashauri ya mji wa Njombe kudumisha umoja wao ili kuepuka matukio ya mauaji, kwani kunapotokea migogoro wahalifu ndiyo wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya mauaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live