Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva bodaboda achinjwa mkewe akishuhudia

Kisuu Dereva bodaboda achinjwa mkewe akishuhudia

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: Habarileo

Watu wasiofahamika wamemchinja dereva wa bodaboda Sadick Mwashambwa (24) akiwa na mkewe na mtoto wao mchanga. Mauaji hayo yalifanyika usiku wa kuamkia jana saa 11.20 usiku katika kitongoji cha Kamficheni kata ya Hasamba wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Inadaiwa kuwa wanaume wawili walikwenda nyumbani kwa Mwashambwa wakavunja mlango na kuingia hadi chumbani wakamkuta akiwa amelala na mkewe na mtoto wao mchanga, wakamkamata na kumchinja mbele ya mkewe. Mtendaji wa kata ya Hasamba, Imma Sichinga na mwenyekiti wa kitongoji cha Kamficheni, Justin Ngondo walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Ngondo alisema alipata taarifa kutoka kwa jirani wa marehemu na baada ya hapo aliwafahamisha wajumbe wa serikali ya kijiji ambao kwa pamoja walifika eneo la tukio na kujionea unyama uliofanyika.

“Mke wa marehemu ambaye kwa wakati mwingi alionekana kutokuwa sawa alitueleza kuwa wauaji wa mumewe walikuwa wanaume wawili na kwamba waliingia ndani kwa kuvunja mlango na baada ya hapo walimchinja mbele yake na kisha kutoweka bila kuchukua chochote” alisimulia Ngondo alisema alimfahamisha mtendaji wa kata, Sichinga ambae aliwataarifu polisi.

Chanzo: Habarileo