Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva ampigia magoti Waziri Simbachawene

Simba Chawene dereva wa Basi akiwa kampigia magoti Waziri Simba Chawene

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, jana majira usiku, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simba Chawene alionekana maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani, akifatilia mwenendo wa usalama barabarani katika eneo hilo.

Akiendelea na zoezi hilo akiwa kaongozana na askari wa usalama barabarani, walimkamata dereva wa basi lilitambulika kwa jina la Sauli, kwa kosa la kuvunja sheria za usalama barabarani.

Hata hivyo dereva huyo aliwashangaza watu baada ya kupiga magoti chini huku akimuomba na kumsihi Waziri huyo kumsamehe kwani ilikuwa bahatai mbaya na kuahidi kutorudia tena kufanya vitendo hivyo vya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani

Jeshi la Usalama Barabarani limekuwa likiwasisitiza madereva kuhakikisha wanafuata sheria na misingi iliyowekwa ili kuepusha ajali za barabarani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live