Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva, Utingo waliobaka na kulawiti mtoto miaka sita wakamatwa

Mbaroni Dereva, Utingo waliobaka na kulawiti mtoto miaka sita wakamatwa

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amesema tayari Watu wawili akiwemo Dereva na Utingo wa Basi la Shule ya Starlight Pre and Primary wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti Mwanafunzi wa Kike wa Shule hiyo mwenye umri wa miaka sita.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa juu wawili hao kudaiwa kumfanyia ukatili huo Mwanafunzi huyo(jina limehifadhiwa) ndani ya gari la Shule.

DC Gondwe aliyeambatana na Waziri Gwajima, amesema “Tulishatoa elimu kwa Shule za Kinondoni kwanza kufahamu na kutoa huduma bora kwa Watoto na hapa walikuja lakini katika mabasi manne waliyokuwa nayo mawili wameweka matroni lakini mawili wameweka vijana wa kiume moja wapo ndio hilo limetokea la huyu Mtoto, tutasimamia miongozo ambayo imepitishwa na Serikali, la pili kwa hawa waliofanya hiki tumekwisha wakamata na tumewapeleka kwenye vyombo vya sheria na tumewafikisha Mahakamani, wapo Segerea”

Kwa upande wake Waziri Gwajima amesema “Tumeambiwa Mtoto amefanyiwa amebakwa na kulawitiwa na Dereva na Konda na mmoja anajulikana kwa jina la Anko, hivyo nikaona nimtafute DC tuje hapa kwasababu humo ndani ya School Bus ndio Mtoto amefanyiwa huo ukatili na Wanaume wawili , anachukuliwa nyumbani wa kwanza anarudishwa wa mwisho wakati wa kurudi gari inapaki wanamfanyia huo unyama kwa zamu leo huyu kesho yule”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live