Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa za kulevya zawafikisha tisa kortini

Fri, 13 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania wakikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana Alhamisi Septemba 12, 2019 na kusomewa shtaka hilo na wakili wa Serikali, Ashurah Mnzava.

Waliopandishwa kizimbani ni Elias Elija Thuran (33), Hassan Mwita Mwimbi (58), Antony Mwiru Kibuyi (28), John Koig Kibuya (40), Felister Kalende Audifes (21), Waziri Mussa Seif (33), Afif Ahmed Afif (34) na Yahya Hussein Nyemba (46).

Akiwasomea shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo,  Mnzava amedai washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi.

Mnzava  amedai Agosti 23, 2019 washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo eneo la Bungoni ndani ya Ilala wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Mnzava amedai siku hiyo washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha bangi kilo 09.65 kinyume na sheria.

Pia Soma

Advertisement
Pamoja na mashtaka hayo, washtakiwa wote  kwa pamoja walikana na  Hakimu alitoa masharti ya dhamana ikiwemo kuwa na wadhamini wawili mmoja kutoka serikalini na mwingine wa kawaida na kuambatanisha na cheki ya Sh10 milioni.

Baadhi ya washtakiwa hao walifanikiwa kukidhi masharti ya dhamana na wengine kurudishwa rumande.

Hakimu Mwaikambo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 26, 2019 kesi itakapotajwa.

Katika kesi nyingine mahakamani hapo, mfanyabiashara na mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Eze Ejike Amosi (38) alifikishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la usafirishaji dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 4.14

Akisomewa shtaka hilo na wakili wa Serikali, Ashurah Mnzava mbele ya Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo amedai mshatakiwa anakabiliwa na kesi ya usafirishaji wa dawa ya kulevya.

Mnzava amedai Agosti 31, 2019 mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo eneo Ubungo Round About wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amedai siku hiyo mshtakiwa huyo alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya heroini kilo 4.14 kinyume na sheria. Mnzava alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi  hiyo hadi Septemba 26,2019 na mshatakiwa alirudishwa rumande.

Chanzo: mwananchi.co.tz