Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dandora: Jambazi hatari asiyeogopa kifo auawa

DONDORAAAA Dandora: Jambazi hatari asiyeogopa kifo auawa

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Eddy, anayefahamika kwa jina la Yutman Mgaza Wadando huko Dandora, alipigwa risasi na askari polisi alipokuwa akiwaibia wananchi.

Jambazi huyo sugo ambaye amekuwa akiingia na kutoka gerezani mara nyingi, alikuwa pamoja na marafiki zake ambao ni wanachama wa genge analoongoza alipouawa.

Maelezo yanaonesha kuwa kijana huyo aliishi kwa upanga na hakluwa na uonga wa kufuata alichotaka kwani hakutishwa na mazingira alimokuwa ndani.

Eddy aliwahangaisha wakaazi mtaani mwake na kando na hayo hakuona haya kujigamba mitandaoni kuhusu ushujaa wake.

Alifanya hivyo licha ya kuwepo kwa polisi hatari kama vile Saigon Punisher na Hessy wa Dandora ambao wanasifika kwa kuwaangusha wahalifu wakali katika makazi duni.

"Tunaamini kwamba alikuwa akisaidiwa na kikundi cha watu ambao walinufaika na njia zake za uhalifu na walikuwa wakimdhamini," duru kutoka polisi zilisema.

Eddy alikuwa mwanachama na mmoja wa viongozi wa genge la kuogopwa liitwalo Wadando na alikuwa ameonywa mara kadhaa kubadili njia zake ila akawa kichwa ngumu.

Mwaka mmoja uliopita, kijana huyo alibanwa kwenye kona alipokuwa akijaribu kuiba pikipiki lakini alitoroka akiwa na majeraha ya risasi.

Licha ya polisi kuwaomba wakazi wa eneo alikokuwa akiishi kutoa ripoti kumhusu, hamna aliyejitokeza. Badala yake alichapisha ujumbe Facebook akijisifu jinsi alivyokwepa kifo.

"Kuzaliwa ni baraka, kufa ni lazima," aliandika.

Hata hivyo, arobaini zake zilifika siku chache zilizopita wakati alienda kwenye mishoni na mmoja wa majambazi wenzake.

Wananchi waliwadokezea polisi ambao walijibu kwa haraka na kumuua jambazi huyo hatari na kumjeruhi msaidizi wake ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Mama Lucy.

Kufuatia shambulizi hilo, maafisa wa polisi walipata bunduki za kujitengenezea ambazo wawili hao walikuwa wakitumia katika shughuli zao za wizi na pikipiki mbili.

“Walahi Eddy umeamua tu hivyo. Iko tu sawa siku moja tutakufa. Mimi siamini Yutman niwewe umetuacha. RIP," mjane wa Eddy aliomboleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live