Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari wa Hospitali ya Amana asomewa mashtaka ya ubakaji, ulawiti

Mwaipolaaaa Daktari wa Hospitali ya Amana asomewa mashtaka ya ubakaji, ulawiti

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dkt. Joseph Mwaipola ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya Amana Mkoani Dar es Salaam, leo Septemba 9, 2022 amefikishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu yakiwemo kumbaka mtoto wa miaka 17.

Shitaka hilo limesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga ambapo mashitaka yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto.

Shtaka la kwanza ni ubakaji, Wakili Sylvia amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 2022 katika Hospitali ya Amana.

Shtaka la pili inadaiwa Mei 31, 2022 akiwa katika nyumba ya wageni ya Pazuri iliyoko Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti huyo.

Shtaka la tatu ni kulawiti, mshitakiwa anadaiwa alitenda kosa Februari 2022 katika Hospitali ya Amana, ambapo alimlawiti binti huyo.

Mshtakiwa amekana mashtaka, upande wa mashitaka umeeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na unaomba tarehe ya kumsomea maelezo ya awali.

Hakimu Roboroga ametoa masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho pamoja na Vitambulisho vya kura au vya kazi watakaotia saini dhamana ya Tsh. milioni tano.

Mshtakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana, hivyo yuko nje kwa dhamana, kesi itatajwa Oktoba 5, 2022 kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali (PH).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live