Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari kortini madai rushwa

MAHAKAMA Daktari kortini madai rushwa

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Singida imemburuza mahakamani Dk. Abdul Sewando wa Hospitali ya Rufani Mkoa wa Singida (Mandewa), akishtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mgonjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 5, 2020 majira ya saa 9.30 alasiri baada ya kuwekewa mtego na kujiridhisha kuwapo kwa tuhuma hizo.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa na maofisa wa Takukuru baada ya kumaliza kumsafisha mgonjwa akiwa eneo la hopitali hiyo.

Elinipenda alisema awali uchunguzi wa Takukuru mkoani hapo ulibaini, Mei 6, 2020 mtuhumiwa alipokea Sh. 60,000 kutoka kwa mgonjwa ambaye jina lake limehifadhiwa ili ampe huduma ya kumsafisha baada ya kumfanyia vipimo vya 'Ultra Sound'.

Alisema uchunguzi wao pia ulibaini kuwa mtuhumiwa alielekeza atumiwe fedha hizo kwa njia ya mtandao na alizipokea kwa njia ya M-pesa kupitia simu yake.

Alitoa tahadhari kwa watumishi wa idara ya afya mkoani humo kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya taaluma zao hususani kipindi hiki ambacho jamii inawategemea kutokana na janga la corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live