Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari kortini kwa kuomba rushwa sh. 10,000 kwa mjamzito

Daktari Mahakamani Daktari kortini kwa kuomba rushwa sh. 10,000 kwa mjamzito

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari wa kituo cha afya kata Nyarugusu wilayani Geita anayefahamika kwa jina la Dk Paul Juvenary wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh 10,000/= kwa mama mjamzito ili wampatie huduma.

Akizungumzia sakata hilo Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU ) Mkoani Geita Leordanas Felix amesema mama huyo mjamzito alifika kwenye kituo hicho cha afya kwa dhumuni la kupata huduma ndipo akapata kikwazo cha kutopewa huduma mpaka atoe rushwa.

Amesema Takukuru walifanya mtego na kumkamata daktari huyo ambaye tayari wamemfikisha mahakamani.

Aidha, amesema wamemkamata mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Bombambili mjini Geita, Richard Kabaigwe kwa tuhuma za kumuomba rushwa mzazi wa mwanafunzi (jina limehifadhiwa) ambaye alifika shuleni hapo kuomba nafasi ya mwanaye kuhamia kwenye shuleni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live