Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari hospitali ya wagonjwa wa akili adaiwa kulawiti

60150 Pic+daktari

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linamshikilia Dk Ame Juma Ame mkazi wa Fuoni Unguja kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 21, akidaiwa kufanya kitendo hicho baada ya kumpa mhusika dawa ya usingizi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Mei 28, 2019 Kamanda wa polisi mkoani humo, Thobias Sedeyoka amesema daktari huyo wa hospitali ya wagonjwa wa akili ya Kidongo Chekundu anaendelea kuhojiwa na polisi.

Amesema aliyefanyiwa kitendo hicho alikwenda kwa daktari huyo kwa ajili ya kuomba kulipiwa ada.

“Kwa sababu ulikua muda wa jioni katika maandalizi ya futari mtuhumiwa alitumia fursa hio kumuwekea dawa kijana huyo na kufanya kitendo hicho baada ya kupoteza fahamu,” amesema Sedeyoka.

Chanzo: mwananchi.co.tz