Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari anayedaiwa kuua kwa kumtoa mimba mwanafunzi apatwa kigugumizi kizimbani

70231 Daktari+pic

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam, Dk Emmanuel Kawacha ambaye ni mkazi wa Kibo, Kinondoni  Jijini Dar es Salaam Tanzania, jana alijikuta akishindwa kujitetea baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kujibu shtaka linalomkabili.

Akisomewa vielelezo vinane mahakamani hapo Leo Agosti 6, 2019, mbele ya Hakimu, Caroline Kiliwa, Wakili wa Serikali, Neema Moshi alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na shtaka la kuua bila kukusudia baada ya kumtoa mimba mwanafunzi wa chuo aliyetajwa kwa jina la Lightness Jeremia.

Wakili Moshi alidai kuwa mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 5, 2013 eneo la Kibo, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Deus Njau aliyempatia mimba Lightness aliithibitishia mahakama kuwa, Marehemu aling’ang’ania kuitoa mimba hiyo kwa sababu zake binafsi licha ya yeye kumkataza asifanye hivyo.

Hata hivyo, Hussein Mohammed aliyekuwa rafiki wa Lightness aliiambia  Mahakama kuwa alimpeleka Lightness kwa Dk Emmanuel baada ya  kumuomba amtafutie daktari wa kuitoa mimba hiyo.

Hata hivyo, mshtakiwa alipotakiwa ajitetee alishindwa baada ya kuzungumza mambo ambayo hakuulizwa mahakamani hapo.

Pia Soma

Hakimu Kiliwa aliahirisha kesi hiyo na mshtakiwa amerudishwa rumande.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz