Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dairy ya shahidi yaahirisha kesi ya kina Mbowe

Mbowe Kesi 2 Pic Data Dairy ya shahidi yaahirisha kesi ya kina Mbowe

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu imeahirishwa baada ya malumbano ya kisheria kuibuka katika mahakamani kuhusiana na uhalali wa shahidi kupanda kizimbani akiwa na diary, simu na kalamu.

Upande wa utetezi unadai kuwa shahidi huo alikuwa anatumia vifaa hivyo wakati akitoa ushahidi wake Ijumaa, jambo wanalosisitiza kuwa ni kinyume cha sheria na utaratibu.

Jaji Joachim Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumanne kwa ajili ya kutoa uamuzi mdogo kuhusiana na mvutano huo.

Mvutano huo wa hoja za kisheria umeibuka muda mfupi baada ya mahakama kutoa uamuzi wa pingamizi lililoibuliwa na mawakili wa utetezi Ijumaa wakipinga barua ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, ambayo shahidi huyo aliiomba mahakama iipokee kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Wakili Mtobesya: Kifungu namba 264 cha CPA, hapo awali tulisimama na kusema hili ni shauri la uhujumu uchumi, kwenye sheria hiyo hakuna nguvu inayotupatia kile tunachotaka kufanya.

Lakini kifungu namba 28 cha CPA, ndio kinatumika kwenye hiyo hoja tuliyoiwasilisha.

Sasa basi kifungu 264 cha CPA kinatumika kwa wakati huu kwenye hili hoja tuliyoiwasilisha.

Wakili Mtobesya: Naomba itoshe kusema tunaomba mahakama ifanye tulichoomba kufanya na ikubaliane na maombi yetu

Lakini wakati tunawasilisha tulielezwa vitu vilivyotokea mahakamani na vilionekana hakuna ubishi Shahidi alikuwa na diary na ikawekwa chini ya ulinzi wa mahakama na hajapinga

Wakili Mtobesya: Kitu kingine ambacho hawapingi ni wakati shahidi anaongozwa hakuna wakati wowote aliomba kuwa na diary kizimbani.

Wakati anaongozwa kwenye ushahidi wake hakuna sehemu alipoimba formally na sisi ndio maana tunapinga

Wakili Mtobesya: Kuna hoja iliongelewa kaka yangu Pius na Chavula hao waliwasilisha kwamba kama Shahidi alikutwa na material yoyote kizimbani, sisi tunasema ziko sababu za kutokumuamini shahidi na sababu akiingia na diary kwa kificho na akajisahau akaifungua kwa kificho.

Wakili Mtobesya: Kifungu kilichotumika kwenye PGO 282 hakijaelekeza kama shahidi atatakiwa kuja na diary kama ni kufanya kumbukumbu anaweza kufanya hata nyumbani na hata akija nayo anaweza kuiacha nje ya mahakama. Kwahiyo maombi yetu ni kwamba vifungu hivyo havisemi hivyo.

Kifungu kinachonipa tabu ni katika PGO hiyo hiyo kwenye kile kifungu alichosema not book haiwezi kukaguliwa na mtu mwingine yoyote.

Wakili Mtobesya: Kama hivyo ndiyo maelezo yake shahidi aki refresh memory kwa namna hiyo inamaana mshtakiwa hata pata haki yake.

Kwa kusema hayo muheshimiwa Jaji na yale tuliyowasilisha mwanzo mahakama itupatie unafuu kwa yale tuliyoyaomba

Wakili Peter Kibatala: Upande wa mashtaka hakuna hata mmoja aliyezungumzia kilichopo kwenye diary, ili mahakama ijue material yatolewe na Shahidi

Wakili Kibatala: Katika kifungu 264 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kilishawahi kuamuliwa na mahakama hii wakati wakiomba kufanya marekebisho kwenye nyaraka mbalimbali

Kifungu hiki kina hakikisha mahakama haifungwi mkono, ukienda kifungu cha 127 kinatoa katazo.

Hapa swali ni kwamba shahidi alikutwa na diary au hakuwa nayo ili kuondoa mlolongo wote kwanini tusiangalie kilichopo ndani lakini mawakili wa Serikali hakuna hata mmoja aliyejibu hiyo hoja.

Wenzangu hawajagusa PGO 282 5 na 6 lakini wamekimbia kwenye saba na nane Sheria imewekwa wazi ni vitu gani vinavyotakiwa kuwepo.

Kiapo kinaisha pale Jaji anaposema asante na kwaheri lakini kusema ilitokea wakati wa uwasilishwaji sio sahihi.

Hawezekani sheria ikasema material ya kutumika mahakamani iwe siri ya shahidi tu ndio maana tumeomba wote tuangalie nini kilichopo ndani.

Wote ni mashuhuda diary ilikutwa lakini hakuna wakili aliyesema aliomba ruhusa bado tunasisitiza tunataka diary ifunguliwe tuone nini kilichopo.

Washtakiwa wana kesi ya ugaidi wanataka kuona ushahidi wa nguvu uliotangazwa sio mashahidi wanaokutwa na diary halafu inatumika nguvu kubwa kumuokoa tunaomba mahakama itolee uwamuzi yale tuliyoyaomba ndio hayo tu Mheshimiwa.

Chanzo: mwananchidigital