Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dada wa saluni auawa kwa mganga

Screenshot 20220225 212220 Facebook Dada wa saluni auawa kwa mganga

Fri, 25 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Kigoma wanamshikilia Mwendesha Bodaboda na Mganga wa kienyeji wote Wakazi wa Kasulu kwa tuhuma za kumuua na kumzika Mwanamke aliyekuwa akifanya kazi saluni Kasulu ambapo mauaji hayo yalitokea baada ya Mwanamke huyo kwenda kwa Mganga na pesa zaidi ya milioni 9 akitaka zizindikwe ili apate pesa nyingi zaidi ya hizo.

Kamanda wa Polisi Kigoma ACP Jemes Manyama amesema Dada huyo Lidya Kamala Soka (42) Mkazi wa Murusi hakujulikana aliko kwa wiki moja tangu tarehe 16 ambapo baadae ilibainika alipigwa na kitu kizito kichwani na kunyongwa kabla ya kuzikwa eneo la porini la Kagondo Wilaya ya Kasulu.

Amesema Marehemu alihitaji kupata tiba ya asili ya kuzindika fedha kwa ajili ya biashara zake kwa Mganga wa kienyeji na kuamua kumkodi bodaboda kwenda na pesa hizo milioni tisa na laki tano ili ziweze kuongezeka katika bishara zake.

"Baada ya kumuua marehemu walichimba shimo lenye urefu wa futi tano na kumfukia ili asionekane lakini baada ya kuhojiwa na kubanwa na Polisi walikiri kumnyang'anya pesa hizo, upeleezi wa kesi hii unaendelea kubaini Wauaji wengine walioshirikiana na Watuhumiwa kisha watafikishwa Mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live