Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DPP awafutia kesi wanaodaiwa kusababisha hasara NFRA

Mahakama Mahakama DPP awafutia kesi wanaodaiwa kusababisha hasara NFRA

Thu, 19 May 2022 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi na kuwachia huru, watumishi wawili wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA), Mohamed Mzingi na Peter Tarimo, waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuisababishia NFRA hasara ya Sh977milioni.

Ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama hiyo, kuwa hana nia ya kuendelea na shtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Mzingi na Tarimo, wanadaiwa kukiuka kanuni ya ununuzi kwa kuingia mkataba na kampuni ya Bajuta Internation Ltd, ambayo haikukidhi vigezo kwa kuwapatia zabuni ya kununua maturubai, ambayo yaliharibika kabla ya muda wake.

Washtakiwa hao wamefutiwa shtaka lao jana, chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo, umetolewa leo Mei 19 na Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Wakili kutoka Takukuru, Hassan Dunia aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya usikilizwaji ushahidi wa upande wa mashtaka lakini Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hana nia ya kuendelea na kesi hiyo dhidi ya washtakiwa hao.

Wakili Dunia, baada ya kueleza hayo, Hakimu Kyaruzi amesema kupitia kifungu hicho, mahakama imewafutia shtaka washtakiwa hao na kuwaachia huru.

Hakimu Kyaruzi baada ya kutoa maelezo hayo, washtakiwa waliachiwa huru na kuondoka zao.

Tayari shahidi mmoja wa upande wa mashtaka, alikuwa ametoa ushahidi wake dhidi ya washtakiwa hao.

Shahidi huyo, Cresensia Dominic (52) ambaye ni Mchunguzi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya ya Chalinze, alieieleza Mahakama namna alivyoshiriki kuchunguza maturubaini yalivyoharibika kabla ya muda wake wa matumizi kuisha, baada ya kukiukwa kwa kanuni za manunuzi.

Katika ushahidi wake, Dominic alidai Januari 20, 2017 akiwa Makao makuu ya Takukuru eneo la Upanga, alipokea taarifa kutoka kwa mkuu wake wa kazi ikimuelekeza kufanyia uchunguzi malalamiko ya maturubai yaliyonunuliwa na NFRA kupitia kampuni ya Bajuta Internation Ltd kuharibika kwa muda mfupi.

"Tulianza kwa kukusanya nyaraka 12 kutoka NFRA, Shirika la Viwango nchini (TBS) na kampuni ya Bajuta Internation Ltd, ikiwemo taarifa ya kikosi kazi kilichofanya uchunguzi wa ununuzi wa maturubai na hati ya malipo ya kampuni hiyo," Alidai shaidi

Katika kesi ya msingi, Mzingi na Tarimo wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2021 yenye mashtaka mawili ambayo ni matumzii mabaya ya Madaraka na kuisababishia hasara NFRA.

Chanzo: Mwananchi