Mkurugenzi wa mashtaka nchini DPP amesema hana nia ya kuendelea na kesi namba 11/2022 iliyokuwa ikimkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi ya usafirishaji haramu wa binadamu na kuomba shauri hilo kuondolewa katika mahakama ya Mkoa wa Mwanza
Akisoma maamuzi hayo wakili mwandamizi serikali Dorcus Akyoo alisema DPP alifikia uamuzi huo kufuatia kifungu cha sheria namba 90 kifungu kidogo namba 11 Sura namba 20 cha mwenendo wa mashahidi kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya Mkoa wa Mwanza Boniventure Lema amemuachia huru Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi katika kesi hiyo namba 11/2022
Aidha mara baada ya uamuzi huo wakili mwandamizi wa serikali Dorcus Akyoo aliiomba mahakama kupokea maombi ya serikali juu ya kuomba awe chini ya uangalizi katika kipindi cha miaka mitatu bila ya kujihusisha na masuala yoyote ya uvunjifu wa sheria na amani katika maeneo yake sambamba na kuripoti kwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mwanza mara moja kila mwezi.
Alisema maombi hayo yalitolewa chini ya kifungu cha sheria namba 70 na 72 kifungu kidogo 'e' pamoja na kifungu namba 74 na 370 kifungu kidogo 'a' cha mwenendo wa makosa ya jinai sura namba 20 na kusema kuwa maombi hayo yameambatana na kiapo cha mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Mwanza RCO