Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DPP agoma kuzungumzia maombi ya Rugemalira

97783 DPP+PIC DPP agoma kuzungumzia maombi ya Rugemalira

Tue, 3 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Biswalo Mganga amesema hawezi kizungumzia suala la mshtakiwa James Rugemalira kuhusu maombi aliyoyatoa katika mahakama kuhusiana na mashitaka yanayomkabili. Akizungumza mjini Tabora leo Jumanne, Machi 3, 2020 amesema suala hilo litapata majibu yake mahakamani ambako Rugemalira ametoa maombi yake. Ameeleza kuwa hawezi kusema kama alikuwa sahihi au vinginevyo kutoa maombi yake na kwamba majibu yatapatikana mahakamani. "Siwezi. Kueleza kama alikuwa sahihi au sio kwa aliyoeleza mahakamani na suala la.mahakamani litajibiwa mahakamani," amesema. DPP Biswalo alikuwa na ziara ya kutembelea mahabusu na magereza na kuzindua kamati ya Jukwaa la Jinai Mkoa wa Tabora.

Chanzo: mwananchi.co.tz