Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DPP: Watuhumiwa kesi uhujumu uchumi lipeni madeni

95227 Pic+dpp DPP: Watuhumiwa kesi uhujumu uchumi lipeni madeni

Tue, 11 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amewataka watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokiri makosa na kuingia makubaliano na ofisi yake, kulipa madeni yao haraka kabla hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao kwa amri ya mahakama.

Malipo hayo yanawahusisha watuhumiwa 341 walihusika kwenye kesi 104.

Biswalo ameyasema hayo leo Jumatatu Februari 10, 2020 wakati akikabidhi mali kwa Serikali zilizotaifishwa kutokana na kesi mbalimbali, makabidhiano yanayofanyika katika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.

Amesema licha ya kukusanya Sh12.3 bilioni, fedha hizo hazijumuishi walikiri makosa  na wanatakiwa kuzirudisha serikalini.

“Oktoba 2019 tulikuwa na zoezi ambalo washtakiwa waliingia makubaliano na ofisi ya  DPP  kwa lengo la kukiri makosa yao kupitia utaratibu maalum, kutokana na zoezi hilo kuna fedha Sh12.3 bilioni mpaka tunavyoongea zimelipwa kwenye akaunti maalum na zipo benki kuu."

“Lakini hizi hazijumuishi fedha ambazo watu waliokiri wanatakiwa kuzirudisha kwa hiyo nitumie fursa hii kuwatahadharisha kwamba amri ya mahakama lazima itekelezwe, kwa kuwa tulikubaliana wanatakiwa kulipa hiyo fedha na walipewa kipindi ambacho walitakiwa kulipa lakini mpaka sasa bado hawajalipa,” amesema Biswalo.

Pia Soma

Advertisement
Amesema washtakiwa hao ambao hawajalipa mpaka sasa wanapaswa kurudi kwenye makubaliano waliyosaini ambayo ni amri ya mahakama.

“Kuna kifungu kipo kwa amri ya mahakama kinachoelezea hatua ambazo zitachukuliwa za ziada au kurudisha baadhi ya mashtaka ambayo tuliyafuta niwaombe walipe mapema iwezekanavyo kabla hatua hizo hazijachukuliwa,” amesema Biswalo.

Chanzo: mwananchi.co.tz