Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DPP, Takukuru, DCI waagizwa kuharakisha kesi

Ffada34242434ee84072e8756c1a0a05 DPP, Takukuru, DCI waagizwa kuharakisha kesi

Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

OFISI ya Rais Utumishi na Utawala Bora imeagiza Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI) washirikiane kuharakisha michakato ya kesi.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Deogratius Ndejembi alitoa agizo hilo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki wakati akifunga mkutano wa siku mbili wa wadau wa Jukwaa la Haki Jinai.

“Ofisi ya DPP, PCCB na DCI nendeni mkashirikiane na kufanya kazi pamoja katika kurahakisha mchakato wa kesi mahakamani ili haki za watuhumiwa zipatikane haraka”alisema Ndejembi.

Alisema ushirikiano huo utajionesha kwenye viashiria vikiwemo vya kupungua malalamiko ya kubambikiwa kesi, kuharakisha upelelezi, kesi kupelekwa mahakamani, na kuharakishwa kutolewa hukumu.

Ndejembi aliwataka washiriki wa jukwaa hilo wawasilishe kwa wasaidizi wao maazimio 16 yaliyofikiwa katika mkutano huo kwa utekelezaji.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome aliwataka wajumbe hao washirikiane kuharakisha michakato ya kesi tangu hatua ya uchunguzi hadi kesi mahakamani.

Mwenyekiti wa mkutano huo, DPP Sylvester Mwakitalu alisema viongozi hao wanatakiwa waende kutembelea magereza kuona mahabusu, majarida ya kesi na watoe uamuzi wakiona inafaa.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni alisema kumekuwa na malalamiko ya ukiukwaji wa maadili na kuwepo kwa vitendo vya rushwa.

DCI Camilius Wambura alisema ushirikiano huo ni wa lazima na waache tabia za makusudi kukwakisha utendaji kazi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz