Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED wa zamani na wenzake 11 kortini kwa hasara ya mamilioni

Watumishi Watano Watano (600 X 312) DED wa zamani na wenzake 11 kortini kwa hasara ya mamilioni

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumishi tisa akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda vijijini, Amos Kusaja na wafanyabiashara watatu wa mjini Bunda wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh351.6 milioni.

Washatakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka yenye makosa 34 wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Bunda.

Pamoja na mambo mengine, washtakiwa hao wanadaiwa kuongoza genge la uhalifu na uhujumu uchumi kinyume cha aya ya nne kifungu kidogo cha kwanza jedwali la kwanza na vifungu vya 58 (1) na 60 (2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa kupanga Sura ya 200 na marejeo yake ya mwaka 2022.

Washtakiwa wengine katika shauri hilo namba 17/2023 ni Amanyise Kayange, Mona Bitakwate, Sangi Ruge, Abbas Abdul, Hezbon Bature, Emmanuel Mbonje, Allan Aron, Shaban Ndalu na Nuru Yunge ambao walikuwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Wengine katika shauri hilo ni wafanyabiashara wa mjini Bunda, Thomas Kweka, Gabriel Kunene na Mseti Maswi.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumanne Oktoba 17, 2023, Wakili wa Serikali, Tawabu Issa amedai kwa pamoja, washtakiwa waliandaa na kupokea malipo hewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live