Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED wa zamani Mbozi mikononi mwa Takukuru

80782 Pic+ded DED wa zamani Mbozi mikononi mwa Takukuru

Mon, 21 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Aliyekuwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushotho Kazimbaya Makwega anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tanga kwa tuhuma za ubadhilifu wa Sh300 milioni zinazotokana na upimaji wa viwanja katika shamba la mnazi wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Oktoba 18, 2019, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba amesema Makwega alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya Mbozi kabla kutenguliwa na Rais John Magufuli.

Amesema zipo fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya upimaji wa viwanja na mkataba ulikuwa wa Sh300 milioni ambapo mtuhumiwa kwa kutumia nafasi yake anatuhumiwa kubadilisha baadhi ya vipengele.

Amevitaja vipengele vinavyodaiwa kubadilishwa mkurugenzi huyo ni vile vilivyoitaka Kampuni ya Geoplan (EA) ya jijini Dar es Salaam kuweka kiasi cha gharama kwa ajili ya tahadhari ikiwa itachelewa kukamilisha kazi ile gharama itakatwa.

 

Amesema kila mkataba unakuwa na taratibu zake na kwamba Makwega  kwa kutumia nafasi yake anatuhumiwa kujaribu kubadilisha baadhi ya vipengele jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

Pia Soma

Advertisement
Kamanda huyo wa Takukuru amesema mkataba huo wa upimaji ulitakiwa uanze Juni  28 mwaka 2013 hadi Agosti 28, 2018 kitu ambacho hakikufanyika hadi Desemba 3, 2018 ambapo muda ulikuwa  kinyume na taratibu za mkataba na hata fedha za dharura zilizotakiwa kukatwa kama kipengele cha 44 kinavyoonyesha hazikukatwa.

Amesema kwa mujibu wa taratibu za mkataba, kampuni hiyo haikutakiwa kulipwa fedha zote kwa ajili ya mradi huo na mtuhumiwa huyo kwa kutumia mamlaka yake aliidhinisha kampuni hiyo kulipwa fedha zote kama imemaliza kazi zote kinyume cha taratibu.

Amesema kampuni hiyo kama iliidhinishiwa Sh200 milioni na kodi halali zilizotakiwa kulipwa serikalini zaidi ya Sh9 milioni hazikulipwa na ni kinyume na taratibu za mkataba.

Hata hivyo, amesema kasoro hizo inatafsiriwa mtuhumiwa alitumia madaraka yake ya uongozi vibaya kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa sababu hiyo ameisababishia serikali hasara kwa kukosa kodi ambapo amesema kuwa hiyo ndio sababu iliyopeleka kumzuia kwa ajili ya mahojiano.

Chanzo: mwananchi.co.tz